Haisameheki na
haisahauliki damu yako italipwa kwa vyoyote iwavyo...R.I.P mwenyekiti
wangu.......
bdul Mluya shared Iddy Harnaa Mkwama's photo.
Haisameheki na
haisahauliki damu yako italipwa kwa vyoyote iwavyo...R.I.P mwenyekiti
wangu.......
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA SIRI NZITO YA KIFO CHA
MCHUNGAJI CHRISTOPHER REUBEN MTIKILA
Ndugu Wana-Habari,
Kabla sijawaeleza kilichonilazimisha kuwaomba kuongea nanyinyi,
kwanza niwarudishe nyuma kama miaka saba iliyopita, ndipo maisha ya Baba, Mchungaji,
Mwenyekiti na mume wangu, Mchungaji Christopher Reuben Mtikila yalipoanzwa
kuwindwa:-
MAUWAJI YA MHESHIMIWA CHACHA ZAKAYO WANGWE
Mara tu baada ya kifo cha mbunge huyo, mchungaji Mtikila alitoa
ripoti maalumu juu ya mauaji yake ambayo ilimjengea uadui kati ya baadhi ya
vyama vya siasa pamoja na wafanyabiashara wakubwa ambao hadi leo ni wapinzani
wa serikali hapa nchini. Mchungaji Mtikila hadi anafikwa na mauti aliendelea
kupata upinzani wa aina hiyo hiyo kwa sababu mchungaji Mtikila aliendelea kudai
haki ya marehemu Chacha Zakayo Wangwe.
MAUAJI YA BULIGI
Hii ilimwongezea uadui baada ya kusema/kuandika ukweli juu ya
watutsi wa nchi jirani kuvamia nchi yetu kwa mtindo wa kujifanya wafugaji wasio
hama. L.I.F. ilibaini uharamia huo kuwa hawakuwa wafugaji bali walikuwa askari
wa Jeshi la Rwanda waliokuwa na mpango wa kutumika na Chama kimoja cha siasa
hapa nchini ili kuleta mapigano yatakayo zaa mapinduzi. Jambo hili
lilisababisha Rais wa Rwanda, Paulo Kagame kutamka hadharani kuwa angemkamata
Mwenyekiti wa chama chetu cha DP kwa lengo la kumuua na Serikali yetu inajua
hilo. Mara baada ya ripoti hiyo kutolewa na Mchungaji Mtikila "operation
Kimbunga" ilizaliwa na kuponya nchi yetu; lakini chuki na uadui uliendelea
dhidi ya Mchungaji Mtikila.
MCHAKATO WA URAIS NDANI YA CCM
Ikumbukwe kuwa mara baada ya mchakato wa kutafuta mgombea urais
kwa tiketi ya CCM kuanza DP ilitoa ripoti iliyowahusu wagombea sita wa CCM
waliotumia mapesa mengi na kuanza kampeni kabla ya muda na kusisitiza kuwa
Lowasa ni mtu asiefaa kuwa Rais wa nchi yetu. Na baada ya kuhama CCM,
Mwenyekiti wetu aliendelea kutoa tahadhari hadharani jinsi Lowasa asivyofaa
kuwa Rais wa nchi yetu hivyo likaendeleza uadui wake na Chama.
VITISHO KUANZA
Mchungaji Mtikila alipata nafasi ya kuongea katika kipindi
kinachorushwa na STAR TV cha asubuhi "TUONGEE" ndipo alipoanza kupata
vitisho toka kwa watu mbali mbali wengine kupitia kwenye simu wengine uso kwa
uso. Kipindi cha kwanza kilirushwa tarehe 25/9/2015 na kufuatwa na cha tarehe
27/9/2015. Alipotoka studio hiyo asubuhi ya tarehe 27/9/2015 ndipo watu
waliodai wametumwa na Mhe. Edward Ngoyai Lowasa na Mhe Frederick Sumaye
walimuomba wampe nusu bilioni na apewe maovu ya mgombea urais wa CCM ili
afunike alivyowamaliza wao. Mchungaji Mtikila aliwapuuzia mbali wale wajumbe
waliyotumwa kwni aliawaambia kuwa yeye siyo malaya wa kuuza utu wake kwa tende
na haluwa. Yakumbukwe kuwa mahojiano kwenye hivyo vipindi viwili kwenye STAR TV
hayakuwa yanatetea mtu au chama yalikuwa yanatetea Taifa letu lipate Rais
anayefaa. Kwa hiyo basi wale waliochukizwa na mahojiano hayo ni wale amabo
hawakubaliani na mawaidha ya Mchungaji Mikila aliyokuwa anawatahadharisha
watanzania juu ya Mh. Lowasa kuwa hatari kwa usalama wa taifa letu kama atakuwa
Rais wa nchi yetu. Hao watu ndiyo waliopanga mpango mzima wa mauaji ya Mh.
Mtikila ambaye ni mume wangu. Wakati yuko Bunda mjini watu wasiofahamika
walimfuatafuata na tarehe 26/9/2015 gari lake lilifukuzwa na gari usiku wakati
alipokuwa anatoka Bunda kwenda Mwanza kufanya mahojiano ya tarehe 27/9/2015 na
Star Tv.
MPANGO WA MAUAJI HALISI
Mchungaji Mtikila alitafutiwa gari na Victor James Manyahi
ambayo ilikuwa na madereva wawili. Mchungaji madereva hakuwajua. Hata mimi
madereva hao sikuwajua wala sikuwaona. Walikodiwa kutoka wapi sijui, wala sijui
wanafanana vipi. Na wala sijui Victor Manyahi alikodi gari hilo kwa nani na
makubaliano yepi sijui. Kwa hivyo basi, kwenye gari aliyosafiri nayo Mchungaji
Mtikila kulikuwamo madereva wawili na Mgaya Patrick (tunayemfahamu). Wakati
wanakwenda gari lilipata ajali Makambako. Wakati wanarudi wakapata “ajali”
Msolwa Mchungaji akapatwa na mauti peke yake. Ajali ilikuwa mbaya sana IKAUWA
MTU MMOJA AMBAYE NI MCHUNGAJI MTIKILA NA HAKUKUWA MAJELUHI HATA MMOJA. Cha
ajabu kwangu n kuwa mtu ambaye alikuwa ni mlinzi wa kujitolea (body guard)
Mgaya Patrick sijawahi kumuona usoni mwangu kabla na hata baada ya mazishi kuja
kuniambia kilichotokea eneo la ajali. Pamoja na juhudi zangu zote za kumpigia
simu mara kadhaa aje anijuze Mgaya Patrick hajatokea hadi sasa ndugu zangu
wanahabari ninapoongea nanyi. Lakini si kwamba huyu mtu hayupo, yupo lakini
sijaonana naye, kwa nini sijui. Je ndugu zangu wanahabari nimuweke Mgaya
Patrick kwenye fungu gani?
Ndugu Wana-Habari, baada ya kuwaelezea yote hapo juu nakuja
kwenye suala nililowaomba nikutane nanyi ili niongee mbele yenu kuwa
sikubaliani na uchunguzi kuwa Mchungaji Christopher Reuben Mtikila amekufa kwa
ajali. Sikubaliani na kazi ya Polisi kuwa wamefunga file lao kutokana na
Post-mortem report kuwa mauti yaliotokana na ajali. Nafuta kabisa taarifa
iliyotoka katika gazeti la Nipashe chini ya kichwa cha habari kuwa “FAMILIA
YAFUNGUKA KIFO CHA MTIKILA”-ilitolewa mapema mno. Kila mwanafamilia alikuwa
hajawa tayari kutoa kauli yoyote. Kwa niaba ya Chama na familia ya Mchungaji
Christopher Reuben Mtikila naomba tusaidiwe yafuatayo kusudi haki ya mpendwa
wetu ionekane inatendeka:-
Kwa sababu mtandao umeanza kuficha ukweli ili kulinda wauaji;
tunaomba Mheshimiwa Rais aingilie utata wa kifo cha Mheshimiwa Mchungaji
Christopher Reuben Mtikila kwa kuunda tume ya uchunguzi isiyohusisha
polisi.Tunaiomba mamlaka ya mawasiliano yaani Tanzania Communications
Regulatory Authority, TCRA itusaidie yafuatayo:-
(a) Mtu aliyeweka picha kwanza alfajiri kuonyesha mauti ya Mhe
Mchungaji Mtikila alikuwa wapi? Kwenye tukio? Au ni hao wauaji walikuwa wanatoa
taarifa kwa waajiri wao kuwa wamekamilisha kazi!
(b) Mtu aliyeweka picha ya Dr. Jean-Bosco Ngendahimana kwenye
mtandao kuwa ndiye anahusika na mauti ya Mhe. Mch. Mtikila na kumusingizia kuwa
amekamatwa na polisi akiwa anajiandaa kukimbia;
(c) Wote wanaoendelea kumhusisha Dr. Jean-Bosco Ngendahimana na
mauaji ya Mhe. Mchungaji Mtikila, tuwafahamu ili watueleze vizuri.
Ukweli na haki ni vya Mungu hakuna anayeweza kuviua au kuvizuia.
Tunategemea Mungu atawatumia watendaji wa Serikali/nchi yetu wenye nia njema,
na makusudi yaliyonyooka kwa ajili ya nchi yetu ili Mhe. Mchungaji Mtikila
apewe haki dhidi ya wauaji wake.
Asanteni,
Georgia C . Mtikila,
KM DP/Msemaji-Familia